Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya hiyo imetoa taarifa rasmi ya kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, huku ikisisitiza kuwa:
“Wajibu wetu wa kihistoria ni kushikamana, kuelimishana, na kupambana kwa vitendo.”
Sasa ni wakati wa kuchukua hatua zifuatazo:
Vyombo rasmi na mbadala vya habari duniani vishirikiane na kusaidiana katika kufichua ukweli, kutoa elimu kwa umma, na kuzalisha maudhui ya pamoja yanayoanika jinai za Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani kwa jinai hizo.
Wanaharakati wa kisiasa na kitamaduni waandae maandamano ya kitaifa na mikusanyiko ya kimataifa ili kuweka shinikizo kwa tawala za Kiarabu na za Magharibi zinazoshirikiana na utawala huo katili, na kuzitaka zikate mahusiano yao na Israel. Aidha, wachukue hatua ya kufunga kabisa jalada la "kurekebisha uhusiano" na utawala huo, na kuzuia kufunguliwa kwa ubalozi wa Kizayuni katika nchi yoyote ya Kiislamu.
Waislamu na wanyonge huru duniani kote wasusie bidhaa zote za Kizayuni na Kimarekani ili kuivunja nguvu ya kiuchumi ya wachochezi wa vita.
Mashirika ya kijamii na kitaaluma yashirikiane na vyama vya kiraia katika kuendesha migomo ya kisekta, maandamano ya amani, na mashinikizo dhidi ya serikali zinazoshirikiana na utawala wa Kizayuni, ili kuzima kabisa mishipa ya uhai wa utawala huo unaoua watoto.
Maoni yako